IQNA

'Mwamko wa Kiislamu Haujafika Mwisho'

9:30 - December 11, 2012
Habari ID: 2461685
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya kimataifa ya mwamko wa Kiislamu Dakra Ali Akbar Velayati amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba mwamko wa Kiislamu haujafika mwisho wake bali uko mwanzoni mwa njia na unahitajia juhudi maradufu kwa ajili ya kukamilisha mafanikio yake.
Ameashiria njama zinazofanywa na ubeberu wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na kigezo cha serikali ya Kiislamu na kuongeza kuwa, propaganda za kuchafua jina la Uislamu na kuyavunjia heshima matukufu ya kidini ya Waislamu kwa kisingizio cha uhuru wa kusema na kujieleza ni sehemu ya njama hizo.

Katibu mkuu wa Sekretarieti ya Mwamko wa Kiislamu amesema wimbi la mwamko wa Kiislamu lililoanza mwishoni mwa mwaka 2010 ambalo sasa linakaribia awamu yake muhimu na harakati ya mwamko wa Kiislamu ambayo inashirikisha wananchi, vyama vya Kiislamu na wasomi sasa imevuka mipaka ya nchi na kuingia katika upeo wa kimataifa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Velayati ameashiria ushindi wa wanamapambano wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kusema wanamapambano hao wamedhirisha wazi udhaifu wa utawala ghasibu wa Israel na kuulazimisha kusitisha mashambulizi.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Dakta Ali Akbar Salehi pia amehutubia Mkutano wa Kimataifa wa Wahadhari Waislamu wa Vyuo Vikuu na kusema mfumo wa kibeberu unataka kuparamia wimbi la mabadiliko yaliyotokea Mashariki ya Kati na kushika hatamu za kuongoza mabadiliko hayo lakini mwamko wa Kiislamu umekuwa na taathira katika matukio hayo. Amesema wahadhiri Waislamu wa vyuo vikuu wana nafasi na mchango mkubwa katika kuzindua fikra za watu na mchango huo unapata umuhimu mkubwa zaidi katika zama za sasa kuliko kipindi chochote kingine.
1150949
captcha