Mikanda ya video iliyopatikana hivi karibuni inawaonyesha magaidi wa Kisalafi wanaojulikana kwa jina la ' Jeshi la Ukombozi wa Syria' wakichoma moto na kuharibu Misikiti katika mji wa Adlib ulioko kaskazini magharibi mwa Syria. Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa, magaidi kadhaa wameangamizwa na silaha zao kuchukuliwa ngawira kwenye mapigano makali yaliyojiri jana kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaobeba silaha katika eneo la Jabal AbdulAziz magharibi mwa al Hasaka. Tokea mwezi Machi mwaka 2011, magaidi wa Kiwahabbi nchini humo wakiungwa mkono na Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel, Uingereza, Ufaransa na baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na Uturuki walianzisha mapigano na machafuko kwa shabaha ya kuuangusha utawala wa Rais Bashar Assad wa nchi hiyo. Rais Assad anasakamwa kutokana na misimamo yake ya muda mrefu ya kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.
1153714