Kongamano hilo la siku mbili ambalo limemalizika leo limehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi za Kiislamu duniani. Katika ujumbe wake kwa kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Profesa Ekmeleddin Ihsanoğlu amesema kuna haja ya kuimarisha utalii wa kiafya katika nchi za Kiislamu. Katika ujumbe huo uliosomwa na Basir Arsalan, Ihsanoğlu amesema kuimarisha afya katika nchi za Kiislamu ni moja ya malengo ya OIC.
Mada zilizojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na uwekezaji na teknolojia katika sekta ya utalii wa kiafya.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 50 za Kiislamu wakiwemo mawaziri wa afya pamoja na wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO).
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa inaongoza katika utalii wa kiafya katika nchi za Kiislamu duniani.
1156885