IQNA

'Iran imesimama kidete dhidi ya maadui'

11:04 - December 29, 2012
Habari ID: 2471653
Khatibu wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema kuwa, hamasa ya tarehe 30 Desemba mwaka 2009 ilikuwa ishara ya wazi ya kuwa macho na utayarifu wa taifa la Iran wa kukabiliana na njama na fitina ya aina yoyote ile ya maadui yenye lengo la kutoa pigo kwa mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini.
Sheikh Kadhim Siddiqi amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kubainisha kwamba, katika hamasa hiyo ya Desemba 30 mwaka 2009, wananchi wa Iran walikwamisha na kusambaratisha njama za Magharibi zilizokuwa na lengo la kutoa pigo kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na malengo matukufu ya Kiislamu. Ameongeza kwamba, hamasa hiyo ilikuwa pigo kubwa mno kwa maadui wa nje na wa ndani.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, taifa la Iran limesimama kidete na kishujaa katika kipindi chote cha miongo mitatu iliyopita na kuweza kukabiliana na mashinikizo yote na vitisho vya maadui wa Uislamu na maadui wa taifa hili la Kiislamu.

1161856
captcha