IQNA

Imam Khamenei: Ayatullah Tehrani ameacha pengo katika vyuo vya kidini na jamii ya kidini

22:17 - January 02, 2013
Habari ID: 2474784
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Ali Khamenei ametoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Ayatullah Mujtaba Tehrani, mmoja kati ya maraji'i wa kidini hapa nchini na kusema kuwa, kifo cha alimu na mwalimu huyo wa akhlaki kimeacha pengo kubwa kwa vyuo vya kidini, wasomi na jamii ya kidini.
Ayatullahil Udhma Ali Khamenei pia ametoa mkono wa pole kwa ndugu na familia ya wafiwa. Ayatullah Mujtaba Tehrani amefariki dunia hii leo na atazikwa kesho na sala ya maiti ya mwanachuoni huyo mkubwa itaongozwa na Ayatulahil Udhma Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Wakati huohuo, viongozi mbalimbali wa ngazi za juu hapa nchini akiwemo Rais Mahmoud Ahmadinejad, Dakta Ali Larijani Spika wa Bunge, Ayatullah Sadeq Amoli Larijani, Mkuu wa Baraza la Sheria, Ayatullah Mahdavi Kani ambaye ni Mkuu wa Baraza la Wanazuoni linalomchagua Kiongozi Muadhamu na Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Mfumo wa Kiislamu wamemtaja Ayatullah Tehrani kuwa mwanachuoni mkubwa na ameacha pengo kubwa kwenye ulimwengu wa Kiislamu.

1165340
captcha