IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Marekani ndie mfadhili mkuu wa magaidi

17:16 - January 19, 2013
Habari ID: 2482705
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amelaani mauaji ya kigaidi ya Waislamu wa Pakistan, Iraq na Syria na kusema kwamba magaidi wanafanya jinai na kutekeleza malengo ya Marekani katika eneo kutokana na msaada wa fedha na kijeshi wa Washington.
Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kuwa, baadhi ya nchi za Kiarabu pia zinashiriki katika kufanikisha malengo ya Marekani katika eneo na kutenda jinai na mauaji katika nchi za Syria, Iraq na Pakistan. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran aidha amesema, muqawama na kusimama kidete mataifa ya eneo hili dhidi ya njama za Marekani ndiko kutakakoleta ushindi na kwamba maadui wataangamizwa hivi karibuni.

Aidha amebainisha kuwa, mabeberu wa dunia na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel wanapinga dini tukufu ya Uislamu na kutiwa wasiwasi na kuenea mwamko wa Kiislamu katika eneo, hivyo Waislamu wanapaswa kuwa macho na kuimarisha umoja.


1173351
captcha