IQNA

Kufana sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu

14:18 - February 11, 2013
Habari ID: 2494751
Mamilioni ya wananchi wa Iran ya Kiislamu wameshiriki kwa hamasa na shauku kubwa katika maadhimisho ya miaka 34 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadhimisho ambayo yalifikia kileleni jana Jumapili.
Wananchi wa Iran wameadhimisho sherehe za mapinduzi yao matukufu wakiwa wameshikamana barabara, wakiwa kitu kimoja na wakiwa na azma madhubuti zaidi ya kukabiliana na mabeberu wa dunia kupitia kulinda malengo matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu. Waandamanaji katika kila kona ya Iran jana Jumapili kwa mara nyingine walitoa pigo kubwa kwa maadui ambao wanaiwekea Jamhuri ya Kiislamu kila aina ya mashinikizo na vikwazo kwa lengo la kuwafanya wananchi wa Iran wajitenge na mfumo wao huo wa utawala. Hatua ya watu wa matabaka mbalimbali kuanzia wanafunzi wa shule za msingi hadi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na watu wa masokoni, watu wa masuala ya utamaduni na wafanyakazi wa kawaida, wananchi wa kawaida hadi viongozi wa juu wa nchi n.k, ya kushiriki kwa wingi na kwa hamasa kubwa katika maadhimisho ya miaka 34 ya ushindiwa Mapoinduzi ya Kiilsamu, imethibitisha kwa mara nyingine kuwa njama za maadui wa taifa la Iran zimeshindwa. Akihutubia umati mkubwa wa watu waliokusanyika kwenye uwanja wa Azadi hapa mjini Tehran, Rais Mahmoud Ahmadinejad sambamba na kutoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Bahman 22, siku zinapofikia kileleni sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kuwa, mapinduzi haya ni ya wanaadamu wote na si ya Waislamu pekee na wala si ya Wairani peke yao. Mheshimiwa Rais amesisitiza pia kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yameamsha hisia za kimaumbile za wanadamu duniani na kuleta mabadiliko makubwa na ya kimsingi ulimwenguni. Amesema huo ni uhakika usiopingika kwani hata adui mbaya na mkubwa zaidi wa Mapinduzi ya Kiislamu analikiri jambo hilo. Amesema, kwa miaka 34 sasa taifa la Iran liko chini ya vikwazo na mashinikizo ya kila nui ya maadui, lakini mashinikizo hayo yameshindwa kufua dafu mbele ya azma thabiti ya taifa la Iran na kutokana na mshikamano wake na muqawama usiotetereka wa wananchi chini ya uongozi wa busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema mambo hayo kwa kweli yamelifikisha taifa la Iran kwenye kipindi cha dhahabu. Naye Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema mbele ya halaiki ya wananchi walioshiriki kwenye maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Qum (kusini mwa Tehran) kwamba maadui wanapaswa kubadilisha miamala yao. Amesema hivi sasa Iran imezitambua njama mpya za Marekani na kwamba mahudhurio makubwa na yaliyojaa hamasa ya wananchi wa Iran katika maandamano ya kilele cha sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ni udhibitisho kuwa miamala ya kiuadui na mashinikizo ya kisaisa na kiuchumi ya Marekani hayajaathiri chochote katika istikama na kusimama kidete wananchi wa Iran. Kwa kweli hatua ya wananchi wa Iran ya kushiriki kwa mamilioni katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mara zote huwakatisha tamaa maadui ambao wanadhani kuwa kwa kuwawekea mashinikizo ya kila namna wananchi wa Iran, wananchi hao wataacha kuunga mkono mfumo wao wa utawala yaani Jamhuri ya Kiislamu. Mabeberu wa dunia hata wamekuwa wakitamani kuona idadi ya wananchi wanaoshiriki kwenye sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran inapungua, lakini kila mwaka hali inakuwa kinyume kabisa na ndoto hizo za maadui. Kwa hatua yao hiyo, wananchi wa Iran si tu wanawakatisha tama mara zote maadui hasa wa Magharibi, lakini pia wanazidi kuyaamsha mataifa mengine duniani yakiwemo ya Kiislamu kuhusu wajibu wa kupambana na dhulma na ukandamizaji.

1186487
captcha