IQNA

UN yalaani mauaji dhidi ya Mashia Pakistan

15:56 - February 18, 2013
Habari ID: 2498609
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi makubwa yaliyofanywa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika soko moja karibu na mji wa Quetta huko kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Ban Ki Moon amewataka viongozi wa Pakistan kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliokiri kuhusika na mlipuko huo wa bomu. Mlipuko huo ulitokea katika soko moja la kuuzia mboga lenye msongamano wa watu katika eneo la Hazara katika mji wa Quetta.
Watu wanaokaribia 86 waliuawa na wengine wasiopungua 200 kujeruhiwa. Martin Nesirky, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema umoja huo unaunga mkono juhudi za wananchi na serikali ya Pakistan za kukomesha machafuko dhidi ya makundi ya kidini na kikabila nchini humo.
1190697
captcha