Tarehe mosi mwezi huu wa Machi vikosi vya usalama viliwatia mbaroni watu 300 wakiwemo wanawake 15 katika mkoa wa Qassim. Watu hao walikamatwa katika mgomo uliokuwa umeitishwa kwa lengo la kutaka wafugnwa wa kisiasa waachiliwe huru.
Watetezi wa haki za binaadamu wanasema kuna wafungwa 30 elfu wa kisiasa Saudi Arabia. Aghalabu ya wafungwa hao wanashikiliwa pasina kufunguliwa mashtaka. Tokea Februari 2011, maandamano yamekuwa yakifanyika mara kwa mara nchini Saudi Arabia ambapo waandamanaji wanataka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru. Aidha wanataka kuwepo uhuru wa maoni na usitishwaji ubaguzi mkubwa katika nchi hiyo inayotawaliwa na ukoo wa Aal Saud. Baada ya matakwa yao kupuuzwa waandamanaji sasa wanaupinga wazi wazi utawala dhalimu wa Saudia ambapo makumi ya watu wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa na vikosi vya usalama.
1205019