Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanafunzi hao watashiriki katika mashindano haya ya hifdhi, qiraa na tajwid.
Sheikh Ismael Wandeeba, katibu wa Mufti wa Uganda Sheikh Shaban Ramadhan Mubaje amesema wanafunzi hao ni Abubakr Ali Mutebi na Hussein Muwonge ambao waliwasili Kuwait Jumatano iliyopita.
Wanashiriki kufuatia mwaliko aliopokea Mubti Mubaje kutoka kwa Amiri wa Kuwait Swabah Al Ahmadi Al Jabil Al-Sabah kupitia Sheikh Hani Abdul Aziz Hussein ambaye ni waziri wa Waqfu na masuala ya Kiislamu Kuwait.
Wanafunzi hao wanatazamiwa kurejea Uganda Aprili 14 baada ya kumalizika mashindano hayo ya Qur'ani.
Kwa mujibu wa Shirika la Utaifti la Pew Forum idadi ya Waislamu Uganda ni zaidi ya milioni nne katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye idadi ya watu takribani milioni 33. Uganda pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC.
1208673