IQNA

Misikiti 1110 mipya kujengwa kote Iran mwaka huu

11:17 - April 07, 2013
Habari ID: 2515423
Shirika la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA) limetangaza mpango wa kujenga misikiti 1110 mipya katika maeneo mbali mbali kote Iran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Naibu Mkuu wa Shirika la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA) Saeed Sattari amesema misikiti hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka moja ujao katika fremu ya 'Mpango za Zakat'.
Amesema mpango huo ulianzishwa mwaka 2005 kama kwa lengo la kuwajengea misikiti wale wasio na uwezo.
Sattari amesema kuwa tokea mpango huo uanze karibu misikiti elfu sita imejengwa kote Iran kwa kutumia fedha za Zakat na vile vile misaada ya wafadhili na serikali.
Ameongeza kuwa aghalabu ya misikiti mipya itajengwa vijijini kwa kuzingatia mahitajio ya jamii husika.
Naibu Mkuu wa Shirika la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA) ametoa wito kwa wanaojiweza katika jamii kusaidia ujenzi wa misikiti kote nchini.
1208467

captcha