Akizungumza na waandishi habari , Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu Dk Ali Akbar Velayati amesema kuwa, kongamano hilo ambalo litafanyika Jumatatu na Jumanne wiki ijayo litawaleta pamoja Maulamaa 500 wa kigeni na 200 kutoka hapa nchini Iran.
Dk Velayati amesema, kongamano hilo litachunguza matatizo ya nchi za Kiislamu na vile vile changamoto zilizopo katika harakati za Mwamko wa Kiislamu. Aidha ameashiria njama za maadui za kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria na kusema maadui wameanzisha njama hizo baada ya kushindwa kuvunja muqawama nchini humo. Amesema maadui hao wa Uislamu watafeli katika njama zao za kuibua vita vya kimadhehebu nchini Syria. Velayati amesema, Iran inapinga harakati za Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu na kieneo dhidi ya Syria. Amesema Iran inazihesabu njama hizo dhidi ya Syria kuwa ni chuki na uadui dhidi ya Waislamu.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amesema Waislamu na nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua tahadhari ili zisitumbukie katika mtego wa mifarakano ambao umewekwa na maadui.
Dkt. Ali Akbar Velayati ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na ujumbe wa wahadhiri wa vyuo vikuu na mawakili kutoka Misri. Ameongeza kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfumo wa demokrasia ya kidini na kwa hivyo wanaotaka kushiriki katika uchaguzi nchini huchunguzwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Dkt. Velayati ambaye ni mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema sababu muhimu ya kustawi Iran ni irada imara ya wananchi. Ameongeza kuwa kuhuisha thamani, utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu ni nukta muhimu zilizoimarisha Mapinduzi ya Kiislamu Iran na kuipa nguvu nchi hii. Dkt. Velayati ameelezea masikitiko yake kuwa baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati zina dhana potofu ya kwamba, kuwa uhusiano na madola ya kibebebru ndio dhamana ya kubakia tawala zao.
1217030