Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Sheikh Kadhim Siddiqi amesisitizia juu ya mwamko na mshikamano wa Waislamu kwa ajili ya kukabiliana na njama za maadui na vitisho vya mabeberu dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.
Akibainisha matumaini yake kuhusu matokeo ya kikao cha kimataifa kilichopewa jina la "Wasomi na Mwamko wa Kiislamu" kitakachohudhuriwa na wasomi 500 kutoka ulimwengu wa Kiislamu na kitakachofanyika kuanzia tarehe 29-30 mwezi huu mjini Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Siddiqi amesema kuwa, anataraji kuona kikao hicho kinakuwa mwanzo wa kutatuliwa suutafahumu zilizopo katika Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kumaliza tofauti zilizopo. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amezungumzia pia njama za Shirika la Ujasusi la Marekani ,CIA, na Shirika la Ujasusi la Mossad la utawala Haramu wa Israel ,MOSSAD, katika kuwasaidia magaidi na vitisho vinavyowalenga wasomi wa Kiislamu sambamba na kutolewa fatwa zisizo na mashiko na kuongeza kuwa, njama hizo hazina lengo jingine ghairi ya kuzusha mifarakano kati ya Waislamu, kufika kirahisi kwenye masoko ya mafuta na kuziuzia silaha nchi za Kiislamu.
Hujjatul Islam Siddiqi ameashiria taathira chanya ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika ya mwamko wa Kiislamu na kufafanua kuwa, maadui wanataka kuusambaratisha mwamko huo wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, kamwe maadui hawatafanikiwa kwani mwamko wa Kiislamu unazidi kupanuka.
1218264