Safari hizo ziada pia zinalenga kuunganisha mji wa Jeddah na miji au nchi za Afrika kama vile Visiwa vya Komoro, Kinshasa Kongo, Douala Cameroon, Lilongwe Malawi na Johannesburg Afrika Kusini.
Katika taarifa Kenya Airways imesema hivi sasa ina safari mbili kila wiki kuelekea Jeddah na kwamba safari hizo zitaongezeka maradufu kati ya Septemba 3 na Novemba 10 ili kuweza kuwahudumia Waislamu wanaoenda Kuhiji katika mji Mtakafitu wa Makka mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kenya Airways Titus Naikuni amesema safari hizo ziadi zitahakikisha kuwa Mahujaji wa Kenya na kutoka nchi zingine za Afrika wanaopita Nairobi wanasafiri bila tatizo lolote kuekelea Hija.
1246885