Akizungumza mjini Tehran wakati alipokutana na maulamaa wa Iran, Sheikh Rohani amesema serikali inapaswa kutekeleza matakwa ya wananchi na kuhakikisha kuwa maisha yanaboreka.
Rohani amesema kuna haja ya kujiepusha na misimamo ya kufurutu mipaka na kuongeza kuwa, hivi sasa Iran inakabiliwa na matatizo makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika historia.
Kuhusu uhusiano wa wananchi na maulamaa, Sheikh Rohani amesema maulamaa ndiyo ni sauti ya wananchi na ni kama daraja baina ya serikali ya wananchi.
Akiendelea na hotuba yake Sheikh Rohani ameashiria sehemu ya aya ya tisa ya Surat An-Nisaai katika Qur'ani Tukufu isemayo: 'Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa.' Amesema serikali na wanazuoni wanapaswa kuzingatia aya hiyo na kusema maneno yaliyo sawa wanapozungumza na wananchi.
1252168