Ayatullah Ahmad Khatami amewataka wananchi wa Misri kulinda mwamko wao wa Kiislamu na wasiruhusu tena nchi hiyo kuwa mwandani wa utawala wa Kizayuni wa Israel kama ilivyokuwa serikali iliyoondolewa madarakani ya Hosni Mubarak.
Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, wale waliounda serikali iliyopita ya Misri awali walitoa nara za kupambana na utawala ghasibu wa Israel lakini baada ya kushika madaraka walirefusha mkataba wa Camp David na kumwita rais wa utawala ghasibu wa Israel Shimon Perez kuwa ni ndugu yao!
Ayatullah Ahmad Khatami pia ameashiria tukio la kusikitisha la kuuawa Sheikh Hassan Shehata aliyekuwa miongoni mwa maulama wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia nchini Misri na kusema, uwahabi ambao wafuasi wake ndio waliomuua kinyama msomi huyo, ulibuniwa na Waingereza na umeendelea kuwepo kwa kutumia sera za mauaji. Amewataka maulamaa wa Kisuni kupambana na wasababishaji wa mauaji hayo na kutangaza waziwazi kwamba Uwahabi hauna uhusiano wowote na dini ya Kiislamu.
1252920