IQNA

Amri ya kuwakamata viongozi wa Ikwanul Muslim Misri

15:48 - July 11, 2013
Habari ID: 2559919
Mwendesha Mashtaka nchini Misri ameamuru kutiwa mbaroni viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Ikwanul Muslimin akiwemo kiongozi mkuu wa harakati hiyo Mohammad Badie.
Inadaiwa kuwa wakuu wa Ikwanul Muslimin walichochea ghasia za Julai 8 nje ya makao makuu ya kikosi maalumu cha kijeshi kijulikanacho kama Republican Guard mjini Cairo. Katika ghasia zilizoibuka katika eneo hilo, watu 55 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Mohammad Mursi aliyekuwa rais wa Misri aliyepinduliwa wiki iliyopita na jeshi ni kati ya wanachama waandamizi wa Ikwanul Muslimin ambao tayari wameshatiwa mbaroni. Msemaji wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin Gehad El-Haddad amesema kufunguliwa mashtaka Mohammad Badie na viongozi wengine wa ngazi za juu wa harakati hiyo ni njama ya watawala ya kutaka kuvunja maandamano ya wafuasi wa Mursi ambao wanataka arejeshwe madarakani.

Wakati huo huo Ikwanul Muslimin imekataa kuchukua wadhifa wowote kwenye serikali ya mpito. Hii ni baada ya Waziri Mkuu mpya, Hazem El-Beblawi kusema kwamba atawapa baadhi ya nyadhifa za uwaziri niongozi wa Ikhwan.
1256236
captcha