IQNA

Iran yalaani shambulio dhidi ya haram ya Bibi Zainab

16:57 - July 20, 2013
Habari ID: 2564198
Abbas Araqchi msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa katika haram tukufu ya Bi Zainab (AS) huko katika viunga vya Damascus mji mkuu wa Syria.
Araqchi ameziomba taasisi za kimataifa khususan jumuiya za Kiislamu kutekeleza majukumu yao katika kulinda matukufu ya Kiislamu na kufanya juhudi zao zote kuzuia jinai dhidi ya binadamu ambazo ni kinyume na sheria za kimataifa na Kiislamu. Makombora jana yalililenga haram tukufu ya Bi Zainab AS huko katika viunga vya Damascus mji mkuu wa Syria. Makaombora hayo yanasemekana kurushwa na makundi ya magaidi wanaoungwa mkono na nchi za kigeni huko Syria. Serikali ya Syria inasema kuwa machafuko yanayojiri nchini humo yanachochewa na pande za kigeni huku ripoti zikiarifu kuwa magaidi wanaozusha mchafuko huko Syria wengi ni raia wa nchi za nje. Taasisi kadhaa za kimataifa za kutetea haki za binadamu zimetangaza kuwa makundi ya wanamgambo wanaofadhiliwa kifedha na kisilaha na baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo na za Magharibi wamefanya jinai nyingi za kivita huko Syria.
captcha