IQNA

Maandamano ya Siku ya Quds katika nchi 80 duniani

14:56 - August 01, 2013
Habari ID: 2569587
Maandamano makubwa yameandaliwa katika zaidi ya nchi 80 na miji 880 katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo itaadhimishwa Ijumaa.
Mkuu wa Kamati ya Intifadha na Quds nchini Iran Bw. Ramadhan Shariff amesema maudhui ya Siku ya Kimataifa ya Quds ni mwamko wa Kiislamu katika kukabiliana na njama za kutumia mazungumzo ya amani ili kuzuia ukombozi wa Quds Tukufu. Amesema mwaka huu Siku ya Quds inafanyika nchini Iran baada ya hamasa adhimu na ya kudumu ya kisiasa katika uchaguzi wa rais uliofanyika Juni 14. Ameongeza kuwa Siku ya Quds mwaka huu inafanyika katika fremu ya kufichua njama za kishetani za mfumo wa kibeberu katika medani ya matukio ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati hasa nchini Misri na vilevile vita nchi Syria. Ameendelea kusema kuwa, Siku ya Quds pia inaadhimishwa katika kipindi hiki ambacho kuna njama za kutaka kuzusha hitilafu baina ya wafuasi wa madhehebu za Kiislamu na kuvunja mapambano ya Kiislamu dhidi ya Uzayuni.

Shariff pia amelaani mazungumzo ya hivi karibuni baina ya baadhi ya Wapalestina na Utawala wa Kizayuni na kusema mazungumzo haya eti ya amani ni kwa ajili ya kudhamini maslahi haramu ya utawala wa Kizayuni. Ameongeza kuwa uzoefu wa miaka kumi 10 iliyopita umeonesha kuwa, kinyume na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni, maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamekuwa yakifanyika kwa adhama kote duniani.
1266404
captcha