IQNA

Ayatullah Khatami: Muqawama dhidi ya Wazayuni uendelezwe

21:46 - August 02, 2013
Habari ID: 2569899
Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, njia pekee ya kutatuliwa kadhia ya Palestina na kurejeshwa haki za wananchi wa eneo hilo, ni kuendelezwa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Akihutubia umati mkubwa wa waumini walioshiriki kwenye sala ya Ijumaa mara baada ya kumalizika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesisitiza kuwa, hakuna njia nyingine mbadala ya kurejeshwa haki za Wapalestina, isipokuwa kuendelezwa muqawama. Ayatullah Khatami amewatahadharisha Waislamu na njama za Marekani za kuleta mifarakano katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, Marekani inawatumia vibaraka wao wa Kiarabu kuwaua wananchi wa Syria na Iraq, ili iweze kufikia malengo yake haramu katika eneo la Mashariki ya Kati. Akizungumzia kadhia ya Misri, Khatibu wa sala ya Ijumaa ya Tehran amewataka wananchi wa Misri kuwa macho na kuulinda mwamko wao wa Kiislamu na wala wasitoe mwanya kwa Marekani na utawala wa Israel kupora mapinduzi yao. Ayatullah Khatami amelaani vikali uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuliorodhesha tawi la kijeshi la Hizbullah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na kusema kuwa, Hizbullah imesimama kidete katika kuilinda ardhi na wananchi wote wa Lebanon mbele ya vitisho vya utawala wa Israel. Akikumbushia matamshi yaliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba Iran haina lengo la kutengeneza bomu la atomiki, Ayatullah Khatami amesisitiza kuwa, njama za Marekani na nchi za Ulaya za kuzidisha vikwazo dhidi ya wananchi wa Iran, ni kutaka kuuangusha mfumo wa Kiislamu, lakini kwamba njama hizo zimefeli mbele ya irada ya viongozi na wananchi wa Iran.

1266941
captcha