IQNA

Sayyed Nasrallah katika Siku ya Kimataifa ya Quds

'Utawala wa Kizayuni wa Israel lazima uangamizwe'

11:26 - August 03, 2013
Habari ID: 2570157
Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah amesema kuwa, kutokomezwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutakuwa na manufaa kwa wananchi wa eneo lote la Mashariki ya Kati.
Akizungumza Ijumaa mbele ya hadhara ya watu waliokusanyika wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds mjini Beirut, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, kutokomezwa kikamilifu utawala wa Kizayuni wa Israel kutakuwa na maslahi si tu kwa Palestina, bali kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu na Kiarabu. Nasrullah ameelezea lengo la kuhuishwa siku ya Quds na kubainisha kuwa, ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu pamoja na wapenda haki kote duniani hawapaswi kuzifumbia macho haki za Wapalestina. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, utawala wa Israel unahatarisha eneo lote la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa, kipaumbele cha kwanza kinachopasa kupewa katika eneo hili, ni kukabiliana na adui Mzayuni. Sayyid Nasrullah amezikosoa vikali baadhi ya tawala za Kiarabu kwa kudai kuwa, eti Iran ni tishio katika eneo na kusisitiza kuwa, tawala hizo badala ya kugharamika na kutoa fedha nyingi kwa lengo la kuifanya Iran iogopwe katika eneo, zitumie fedha hizo kwa shabaha ya kuikomboa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Imam Khomeini MA aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni siku ya kimataifa ya Quds, kwa lengo la kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika kuzikomboa ardhi za Palestina na Quds Tukufu.
1267059
captcha