Mamia ya wahadhiri wa Vyuo Vikuu, wawakilishi wa majopo ya kielimu na watafiti wa Vyuo Vikuu vya Iran jana alasiri walikuwa na kikao na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ambapo walipata fursa ya kubainisha mitazamo yao sambamba na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali khususan yale ya kielimu na vyuo vikuu.
Mwanzoni mwa kikao hicho, wahadhiri tisa wa Vyuo Vikuu vya hapa nchini walibainisha mapendekezo, ukosoaji na nukta za kuzingatiwa na baadaye Ayatullah Khamenei akaashiria juu ya udharura wa kufanywa jihadi na jitihada zisizo na ukomo ili kufikia maendeleo zaidi na kusisitiza kwamba maendeleo ya kielimu yanaanda uwanja wa kuimarika Iran kisiasa na kiuchumi sambamba na kuwazidishia zaidi izza wananchi wa Iran katika jamii ya kimataifa. Amesema ili kufikiwa lengo hilo kuna haja ya kulindwa na kuboreshwa mjadala wa kielimu, mjadala wa maendeleo ya kielimu na mjadala wa maendeleo ya umma nchini katika vyuo vikuu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa kuweko mitazamo tofauti miongoni mwa wahadhiri wa vyuo vikuu ni jambo lenye kutoa funzo na la kuzingatiwa na akaashiria pia kuhusu upigaji hatua mkubwa wa kielimu hapa nchini na kuongeza kuwa harakati ya kuzalisha elimu na kufanya juhudi kubwa za kufikia maendeleo kulianza tangu karibu miaka 12 iliyopita, harakati ambayo si tu haijasita bali kasi yake imeongezeka. Ayatullah Khamenei amesema harakati hiyo ya kutafuta maendeleo ya kielimu ina umuhimu mkubwa na ni yenye udharura kwa nchi na kwa Mfumo wa Kiislamu.
1269526