Katika kibarua kigumu cha kuwasaili na kuwachunguza mawaziri waliopendekezwa na rais mpya, bunge limefanikiwa kuwapasisha mawaziri 15 wakiwemo wa Wizara ya Usalama, Wizara ya Uchumi na Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Afya na Tiba, Wizara ya Sheria, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Mafuta.
Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limewapigia kura za hapana mawaziri watatu ambao ni Mohammad Ali Najafi aliyekuwa amependekezwa kuongoza Wizara ya Elimu, Mas'ud Sultani Far wa Michezo na Vijana na Ja'far Mili-monfared wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia.
Rais Hassan Rohani pia amemteuwa Dkt. Ali Akbar Salehi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje kuwa Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran.
1273095