IQNA

Bunge la Uingereza lapinga hujuma dhidi ya Syria

6:25 - August 31, 2013
Habari ID: 2582290
Bunge la Uingereza limepiga kura ya kupinga muswada uliowasilishwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron wa kutaka idhini ya kuishambulia kijeshi Syria.
Baada ya vuta ni kuvute kali iliyotawala kikao hicho hapo jana, wawakilishi wapatao 285 dhidi ya 272, walipinga muswada huo na hivyo kutoa pigo kali kwa David Cameron. Baada ya kikao hicho, Waziri mkuu huyo wa Uingereza, alisema kuwa, ni wazi kwamba, bunge linapinga hujuma ya kijeshi dhidi ya Syria. Amesema serikali yake itafuata maamuzi ya bunge kuhusu kadhia hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa Uingereza kupingwa na bunge kuhusiana na suala la kwenda vitani, tangu mwaka 1782.

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, imeonyesha kusikitishwa kwake na mashambulizi tarajiwa ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya taifa la Syria. Katika ripoti yake iliyotolewa jana, wizara hiyo imelaani mashambulizi tarajiwa ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Syria na kusema kuwa, uingiliaji huo wa kijeshi hautakuwa na natija yoyote ghairi ya kuwaua raia wasio na hatia na kuharibu miundo mbinu ya nchi hiyo ya Kiarabu. Afrika Kusini imesisitiza kuwa mgogoro wa Syria unapaswa kutatuliwa tu kwa njia za kidiplomasia. Aidha Pretoria imeonya kuwa, natija ya vita dhidi ya Syria haitabiriki kabisa na kwamba itapelekea hali ya mambo kuwa tete zaidi. Kwa upande wake Gilad Atzmon mkosoaji maarufu wa Kiyahudi amesema kuwa, hivi sasa Rais Barack Obama wa Marekani, amechanganyikiwa kuhusiana na kadhia ya Syria. Amesema Obama hataki kuishambulia Syria, lakini yuko chini ya mashinikizo makali ya Wazayuni suala ambalo limemfanya achanganyikiwe na kushindwa kuchukua uamzi kuhusu suala hilo.
1280140
captcha