IQNA

Imam Khamenei: Iran inakabiliana na tawala za kibeberu

17:58 - September 18, 2013
Habari ID: 2591903
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa changamoto kuu zinazoyakabili Mapinduzi ya Kiislamu hivi sasa, ni kukabiliana na tawala zenye kupenda kujitanua duniani katika jitihada za mapinduzi hayo za kueneza ujumbe wake wa Kiislamu duniani ambao ni kujiepusha na dhuluma.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo Jumanne mjini Tehran alipokutana na makamanda na maafisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kuashiria kuwa, mantiki ya dhuluma na ukandamizaji daima imekuwa ikikabiliana na linganio la kujiepusha na dhuluma, suala lililopelekea mwangwi wa mapinduzi hayo utoke nje ya mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kupokelewa kwa mikono miwili na watu wa mataifa mbalimbali duniani.
Ayatullah Khamenei aliongeza kuwa: "Mfumo wa Kibeberu umeeneza vita, umasikini na ufisadi duniani kwa kutegemea ile mbinu ya kuigawa dunia baina ya dhalimu na wadhulumiwa. Katika kukabuliana na hilo, Mapinduzi ya Kiislamu yanayotegemea mafundisho halisi ya Kiislamu, yamekuja na kusema msiduhulumu wala msidhulumiwe. Nukta hii inapinga kabisa misingi ya ubeberu na hapa ndipo palipo na changamoto."
Aliendelea kusema kuwa Amesema kuwa, ujumbe wa mapinduzi ya taifa la Iran, umekuwa ukipambana vikali na mataifa ya kibeberu, tawala zenye kufungamana nao na mitandao vamizi ya kimataifa, katika hali ambayo utawala wa kimabavu na waitifaki wake, unajitahidi kueneza satwa yake kupitia mambo makuu matatu ambayo ni kueneza vita, umasikini na ufisadi. Amesisitiza kuwa dini Tukufu ya Kiislamu inapambana na mambo hayo na kwamba hiyo ndio changamoto kuu ambayo imekuwa ikiikabili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema kuwa, kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita utawala wa Kiislamu hapa nchini Iran, umekuwa ukikabiliana na matatizo na hujuma mbalimbali za madola ya kibeberu.
Kuhusu uharamu wa silaha za nyuklia, Ayatullah Khamenei alisema: " Sisi hatupingi silaha za nyuklia kwa ajili ya Marekani au wengine, bali tunazipinga kwa ajili ya itikadi yetu. Hatuzukibali silaha hizo na hakuna anayepaswa kuwa nazo. Wakati tunaposema msiwe nazo sisi tunamaanisha kamwe hatupaswi kuwa nazo na wala hatutawahi kuzimiliki….Sababu ya Wamagharibi kupiga kelele kuhusu Iran ya Kiislamu si kwa ajili ya silaha za nyuklia bali wanaipinga nchi hii kwa sababu ndio mhimili mkuu wa mrengo wa kupinga dhulma."
1289652
captcha