Ayatullah Sheikh Makarem Shirazi amesema hayo katika mazungumzo yake na Nikolai Mladenov mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq na kubainisha kwamba, baadhi ya nchi zinalaani jinai za kundi la kigaidi la Daesh lakini katika upande mwingine zinashirikiana na kundi hilo na hata kulisaidia. Ayatullah Makarem Shirazi amesisitiza kwamba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapaswa kuzionya vikali nchi ambazo zinalipatia silaha kundi la kigaidi la Daesh na kununua mafuta yaliyoghusubiwa yanayouzwa na kundi hilo la kigaidi.
Kiongozi huyo wa kidini ambaye pia ni Marjaa Taqlidi amebainisha kwamba, endapo kundi la kigaidi la Daesh litakatiwa misaada na kubainishwa vyema mitazamo ya kundi hilo, hapana shaka katika kipindi cha miezi michache tu kundi hilo litasambaratika.../mh