IQNA

Qatar kustawisha vituo vya Qur'ani

18:00 - February 19, 2015
Habari ID: 2870538
Waziri wa Masuala ya Awqaf na Kiislamu nchini Qatar ameamuru kuundwa Kamati ya Ustawi wa Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Sharq, kamati hiyo itaundwa kwa mujibu wa malengo ya wizara hiyo kuimarisha utendaji kazi wa vituo vya kuhifadhi Qur'ani ili kulea vizazi vya raia wenye kuifahamu Qur'ani, wenye imani na umahiri.
Ghaith bin Mubarak Al Kuwari Waziri wa Masuala ya Awqaf na Kiislamu nchini Qatar ameamuru kamati hiyo kupendekeza njia za kuimarisha vituo vya Qur'ani na pia uratibu wa harakati za Qur'ani nchini humo sambamba na kutumia teknolojia za kisasa katika vituo vya kufunza Qur'ani.
Wizara hiyo imekuwa ikiunga mkono vituo vya kuhifadhi Qur'ani vyenye kuzingatia malezi bora ya vijana.../mh

2865075

captcha