Wataalamu kadhaa walihutubia kongamano hilo siku ya Jumatatu, wakisisitiza kuwa barua hizo ziliamsha vijana nchini Marekani na Ulaya.
Masoud Tavakkoli, mtaalamu wa masuala ya kimataifa, alisema katika barua ya kwanza, Kiongozi Muadhamu alizungumza na vijana wa nchi za Magharibi kuhusu Uislamu, akibainisha kwamba wanapaswa kujifunza kuhusu Uislamu bila ya kusikiliza propaganda mbaya dhidi ya Uislamu.
Vile vile amesisitiza haja ya kutoa mafunzo kwa wataalamu ili kuutambulisha Uislamu katika nchi za Magharibi.
Mohammad Mehdi Ahmadi, mwambata wa zamani wa kitamaduni wa Iran nchini Uhispania, alisema ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ulisababisha dhamiri za vijana wa Magharibi kuzinduka.
Alisema iliunda mjadala dhidi ya mazungumzo ya Magharibi ambayo yanataka kuuonyesha Uislamu kama dini ya vurugu.
Alimnukuu mwandishi mashuhuri wa Uhispania akimwambia kwamba tafsiri ya barua za Ayatullah Khamenei ilionyesha kuwa mitazamo yake ni tofauti na baadhi ya wanaodai kuzungumza kwa jina la Uislamu lakini matokeo ya mwenendo wao ni vurugu na ghasia.
Mwandishi huyo wa Uhispania alibainisha kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu anawatolea wito vijana wa Kimagharibi kujifunza kuhusu Uislamu kupitia vyanzo vyake asilia, yaani Qur’ani, Mtume Muhammad (SAW) na Ahul Bayt (AS), Ahamdi alisema.
Avandar Turkli, mwakilishi wa Shirika la Uchapishaji la Tasneemnchini Uturuki, alikuwa mzungumzaji mwingine katika kongamano hilo.
Alisema baada ya barua za Ayatullah Khamenei kutafsiriwa na kuchapishwa katika lugha ya Kituruki na chapisho hilo lilipata umashuhuri kiasia kwamba Shirika la Uchapishaji la Kawthar nalo pia lilichapisha barua hiyo.
Alitoa wito kwa juhudi zaidi kukuza na kueleza maudhui ya barua hizo.
Kisha, Hossein Mohammadsirat, mjumbe wa kitivo cha Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (AS), alipanda jukwaa na kubaini kwamba baada ya muongo mmoja tangu barua hizo kuchapishwa, uwanja umeandaliwa kwa ajili ya utambuzi wa maudhui yake.
Amesema maandamano ya chuo kikuu nchini Marekani na Ulaya kwa namna fulani ni utimilifu wa utabiri uliotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mwishoni mwa kongamano hilo, tafsiri za vitabu viwili vya Ayatullah Khamenei katika lugha ya Kiurdu, Kipashtu na Kiswidi zilizinduliwa.
Ayatullah Khamenei aliandika barua kwa mara ya kwanza kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini mnamo Januari 21, 2015, kufafanua sababu za juhudi za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya Uislamu.
Baadaye tarehe 29 Novemba 2015, Ayatullah Khamenei alituma barua ya pili kufuatia msururu wa mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa, akifafanua sababu halisi za ugaidi na kuwataka vijana "waweke msingi wa maingiliano yanayofaa na yenye kuheshimika na ulimwengu wa Kiislamu kwa msingi wa elimu sahihi na ufahamu wa kina.”.
3488339