Ayatullah Rafsanjani amesema hayo wakati alipoonana na makamanda na maafisa wa zamani Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, na kuongeza kuwa, kushindwa jeshi lililojizatiti kwa silaha za kisasa kabisa la utawala wa Kizayuni na wanamapambano wa Hizbullah huko Lebanon kunapaswa kuwe funzo kwa viongozi wa Saudia katika mashambulio yao dhidi ya Yemen. Amesema hali katika nchi za Waislamu za Iraq, Pakistan, Afghanistan, Syria, Yemen, Saudia, Bahrain, Misri na Libya ni mbaya sana huku eneo hili likiendelea kushuhudia mizozo, mauaji na mashambulio ya kigaidi sambamba kuanza mashambulizi ya baadhi ya nchi dhidi ya wananchi wa nchi nyingine. Amesema inatia uchungu sana kuona ulimwengu wa Kiislamu umeelemewa na matatizo yote hayo. Ayatullah Rafsanjani aidha amesema: Wayemen ni watu wavumilivu sana, ni watu wanaofanya kazi kwa juhudi, ni watambuzi wa mambo na ni wenye imani thabiti ya dini wanaoipenda mno nchi yao. Amesema, adui yeyote anayelivamia taifa kama hilo hukumbwa na masaibu makubwa. Vile vile amesema kuwa, njia pekee ya kutatuliwa mgogoro wa Yemen ni mazungumzo ya kisiasa na kwamba lawama na madhambi yote yatamuendea kila anayekwamisha mazungumzo hayo.../EM