IQNA

Jinai za Israel

Yemen : Ugaidi wa uoga wa Israel hauathiri azma ya muqawama nchini Lebanon

19:12 - September 18, 2024
Habari ID: 3479451
IQNA - Makundi ya kisiasa ya Yemen yamelaani vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon ambavyo vilisababisha wengi kuuawa shahidi au kujeruhiwa.

Siku ya Jumanne, milipuko iliyosababishwa na vifaa vya mawasiliano visivyotumia waya, vinavyojulikana kama pager, vilijeruhi maelfu ya watu na kuwaua takriban tisa nchini Lebanon, wakiwemo wanachama wa Hezbollah na raia.

Pager ni kifaa cha mawasiliano ya simu kisichotumia waya ambacho hupokea na kuonesha jumbe za alphanumeric au sauti.

Shambulio hilo limezusha hasira katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, ikiwemo Yemen.

Hashem Sharafeddin, msemaji wa serikali ya Yemen amelitaja shambulio hilo kuwa ni jinai ya kikatili na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Amesema hatua hizo zinaashiria kiu ya Wazayuni ya damu na mauaji ya watu.

Pia alitoa rambirambi kwa Harakati ya Hizbullah na familia za wahanga, Al-manar aliripoti.

Taifa la Yemen lina yakini kwamba kitendo hicho cha woga cha Wazayuni kitaimarisha tu azma ya muqawama wa Kiislamu wa Lebanon kuihami Lebanon, Palestina na al-Quds na kuushinda utawala wa Kizayuni, aliendelea kusema.

Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Mohammed Abdul-Salam pia amelaani kitendo cha Israel cha ugaidi na ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Lebanon.

Amesisitiza kuwa, Lebanon ina uwezo wa kuvuka changamoto hizo na muqawama wa Lebanon una uwezo wa kudumisha makabiliano na utawala haramu wa Israel.

Jumuiya ya wanazuoni wa Yemen pia imelaani kitendo hicho cha kigaidi na kukitaja kuwa ni hatua inayolenga kuficha kushindwa na kushindwa kwa utawala wa Israel.

3489949

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hizbullah yemen israel
captcha