Abdul Malik al Houthi alisema katika hotuba yake ya jana usiku kwamba wale wanaodhani kuwa wanaweza kulipigisha magoti taifa la Yemen kwa kutumia mashambulizi ya kijeshi wanaona ndoto za mchana. Amesisitiza kuwa mshambulizi yanayofanyika sasa dhidi ya Yemen yamepangwa na Marekani, Saudi Arabia na Israel. Kiongozi wa harakati ya Ansarullah amesema utawala wa Saudi Arabia ni askari na hadimu wa Marekani na kwamba mashambulizi ya Saudia hayajaweza kuvunja irada na azma ya taifa kubwa la Yemen licha ya upana na ukubwa wake. Abdul Malik al Houthi amesema mashambulizi hayo yanalenga na kuua wanawake, watoto wadogo na watu wazima na kuharibu makazi ya raia, vijiji na miji. Amesisitiza kuwa mashambulizi hayo yanalenga pia miundombinu muhimu na ya kiuchumi ya taifa la Yemen. Ameongeza kuwa hatari kubwa zaidi inayohatarisha Haramu mbili tukufu yaani Makka na Madina, ni Israel na Marekani. Al Houthi amesema mashambulizi hayo yamedhihirisha kinyongo cha utawala wa Saudia dhidi ya taifa la Yemen na amepongeza mapambano na kusimama kidete taifa hilo.
Zaidi ya watu 2500 wameaua na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya taifa la Yemen.../EM