IQNA

UN yaiondoa Israel katika orodha ya 'muuaji wa watoto'

14:00 - June 09, 2015
Habari ID: 3312544
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amekataa kuuweka utawala haramu wa Israel kwenye orodha ya makundi na watu wanaowaua watoto kiholela duniani.

Kwenye ripoti yake ya kila mwaka kuhusu kadhia hiyo, Ban ameashiria kuwa, watoto 557 wa Palestina waliuawa mwaka uliopita kwenye hujuma ya siku 50 ya utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. Pia ripoti hiyo imesema kuwa Israel inaongoza katika kuharibu idadi kubwa ya shule kupitia mashambulizi yake ya anga dhidi ya Wapalestina. Hata hivyo na kwa masikitiko makubwa, utawala ghasibu wa Kizayuni hauko kwenye orodha ya mwisho inayotoa mukhtasari wa makundi ya watu au mataifa yaliyotekeleza mauaji dhidi ya watoto wasio na hatia. Duru za kidiplomasia zinafichua kwamba, Marekani, baadhi ya nchi za Ulaya na utawala haramu wa Israel zilitumia vitisho na mashinikizo ya kisiasa dhidi ya Katibu Mkuu wa UN ili asiiweke Tel Aviv kwenye orodha hiyo. Inaaminika kuwa, rasimu ya ripoti ya Ban Ki-moon ilikuwa na jina la Israel lakini baada ya mashinikizo, jina la utawala huo bandia likatolewa kwenye orodha hiyo inayofahamika kama ‘List of Shame’.../mh

3312434

captcha