IQNA

Waislamu Nigeria waanzisha Radio na TV mpya

18:15 - June 12, 2015
Habari ID: 3313357
Katika jitihada za kueneza mafundisho halisi ya Kiislamu, jumuiya moja ya Kiislamu nchini Nigeria imeanzisha stesheni mpya za televisheni na radio katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

“Tunataka kuleta mabadiliko katika umma wote wa Waislamu kupitia TV na Radio ya Manara. Tunalenga kuwafunza Waislamu watende amali njema na wajiepusha na kuvuruga amani,” amesema Sheikh Bala Lau, mwenyekiti wa Jama’atu Izalatul Bidah Wa Iqamatis Sunnah (JIBWIS). Akizungumza na gazeti ya Leadership siku ya Alkhamisi, Juni 11,  katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wakati wa kuzinduliwa, vituo hivyo vya habari amesema wamechagua jina la Manara Radio na TV .
Amesema mbali na kueneza Uislamu Manara Radio na TV itabuni nafasi za ajira kwa jamii hasa kwa vijana na wanawake.  Amesema pia watatumia Idhaa na Televisheni ya Manara  kukusanya misaada misikitini ili kuwasaidia wasiojiweza katika jamii.
Sheikh Bala Lau amesema pia watatumia chombo hicho cha habari kutoa mafunzo kwa wasiokuwa Waislamu ili waufahami Uislamu.
Idadi ya watu Nigeria inakadiriwa kuwa milioni 170  ambapo Wakriso ni asilimia 40 na Waislamu ni asilimia 55 na wengi wao wanaishi maeneo ya kaskazini mwa nchi.../mh

3313298

captcha