IQNA

Mahakama Bahrain yamfunga Sheikh Salman miaka minne gerezani

0:31 - June 17, 2015
Habari ID: 3315303
Mahakama ya Bahrain imemuhukumu Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa chama cha Kiislamu cha al Wifaq kifungo cha miaka minne jela, baada ya jaji mkuu kutupilia mbali dai lililotolewa na wakili wa kiongozi huyo wa kisiasa na kidini kuhusiana na ushahidi wa uongo uliotolewa dhidi yake.

Awali mwendesha mashtaka mkuu wa Bahrain aliwasilisha tuhuma za kubambikiza zilizokuwa zikimkabili Sheikh Ali Salman ambaye amekuwa akizuiliwa katika korokoro za utawala wa nchi hiyo tangu mwezi Disemba mwaka jana, zikiwemo za kupanga njama za kubadili mfumo wa kisiasa wa Bahrain kwa nguvu, kutishia usalama wa taifa kwa kutumia nyenzo zilizopigwa marufuku, kuwashawishi watu kukiuka sheria na kuwachochea kuchukiana kwa lengo eti la kuibua machafuko na vurugu. Hii ni katika hali amabayo, eneo la mahakama lilishuhudia ulinzi mkali mno leo, kabla na baada ya kutolewa hukumu hiyo, kwa kuhofia radiamali kutoka kwa wananchi wa nchi hiyo wanaotaka Sheikh Ali Salman achiliwe huru. Kwa mujibu wa Abdullah Shamlawi, wakili wa kiongozi huyo, mahakama hiyo imekataa kusikiliza maswali ya upande wa utetezi yaliyoelekezwa kwa mashahidi wa serikali suala ambalo linathibitisha kuwepo dhulma na ukandamizaji katika mwenendo mzima wa kesi hiyo. Kufuatia hali hiyo, maeneo mbalimbali ya Bahrain yameshuhudia maandamano makubwa ya kulaani hatua ya kuendelea kushikiliwa na kufungwa Katibu Mkuu huyo wa chama cha Kiislamu cha al Wifaq. Maandamano ya amani ya wananchi nchini Bahrain yalianza mwaka 2011, wakati wananchi walipomiminika barabarani kulalamikia haki zao za kimsingi za kisiasa na kijamii. Hata hivyo badala ya utawala huo, kuyafanyia kazi matakwa hayo, ndio kwanza umeendeleza siasa za ukandamizaji na mabavu kukiwemo kuwatia mbaroni na kuwahukumu viongozi wa upinzani.

3315171

captcha