IQNA

Waislamu Marekani wamuarifisha Mtume Muhammad SAW

17:31 - June 20, 2015
Habari ID: 3316510
Waislamu nchini Marekani wameanzisha kampeni yenye lengo la kuonesha sura sahini na adhimu ya Mtukufu Mtume Muhammad SAW kwa wafuasi wa dini nyingine duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya On Islam kampeni hiyo ambayo imekuwa ikiendesha shughuli zake tangu mwaka jana, itaanza rasmi Jumamosi ya leo ya 20 Juni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kampeni hiyo inayotoa mwito kwa walimwengu, itaongozwa na kundi la watu kutoka mabara matano ya dunia kwa ajili ya kufikisha vizuri ujumbe huo. Taasisi ya The Islamic Circle of North America nayo itashiriki katika sherehe hizo za mwaka huu. Sherehe za mwaka jana zilizohudhuriwa na wasomi mbalimbali, zilifanyika chini ya kaulimbiu ya 'Nini malengo ya kuishi?' Katika kampeni hiyo ya mwaka huu itakayofanyika chini ya kaulimbiu ya 'Unampenda nani?' walimwengu wataweza kufahamu lengo la harakati hiyo ikiwa ni pamoja na kufikishiwa ujumbe wa Mtume wa Uislamu (SWA). Kampeni hiyo ya kumtangaza Mtukufu Mtume Muhammad (SWA) kwa walimwengu inafanyika kufuatia kuongezeka chuki zinazoenezwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi dhidi ya dini ya Kiislamu. Mbali na propaganda hizo, vitendo vya makundi ya kigaidi yaliyoanzishwa na kulelewa na madola hayo hayo ya Magharibi, ni tatizo jingine linaloshadidisha chuki dhidi ya Uislamu duniani.../mh

3316147

captcha