IQNA

Ripoti ya Umoja wa Mataifa

Utawala wa Kizayuni wa Israel ulitenda jinai za kivita Ghaza

18:44 - June 23, 2015
Habari ID: 3317957
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai za utawala haramu wa Israel huko Ghaza iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imechapishwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala wa Kizayuni wa Israel uletekeleza mauaji ya kutisha dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza kwenye vita vyake vya siku 50 mwaka uliopita. Wapalestina 2, 140 waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa. Ripoti hiyo inasema asilimia kubwa ya Wapalestina waliouawa ni watoto wadogo, wanawake na raia wasio na hatia. Kamisheni ya Umoja wa Mataifa iliyoendesha uchunguzi huo imesema kuwa Israel ilishambulia nyumba za raia, shule za UN, maeneo ya ibada na hospitali jambo linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa. Mwenyekiti wa kamisheni hiyo, Jaji Mary McGowan Davis amesema kuna ushahidi wa kutosha kwamba, utawala haramu wa Israel ulitenda jinai za kivita kwenye hujuma hiyo ya mwaka jana.
Kulikuwa na hekaheka za kidiplomasia kutoka nchi za Magharibi hususan Marekani kujaribu kuzuia ripoti hiyo kuchapishwa.../mh

3317790

captcha