Mkuu wa idara hiyo Abdallah Zekri ametoa taarifa Ijumaa na kusema vitendo na vitisho dhidi ya Waislamu ni zaidi ya 274 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015 katika hali ambayo katika kipindi sawa na hicho mwaka 2014 kulikiwa na visa 72 vilivyoripotiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa.
Amesema idadi hiyo haiakisi ukweli wa mambo kwani kuna idadi kubwa ya Waislamu Ufaransa ambao huhujumiwa kwa sababu ya dini yao lakini hawatoi ripoti kwa polisi.
Zekri amesema hujuma dhidi ya Waislamu zimeongezeka sana Ufaransa hasa baada ya tukio la kigaidi mjini Paris mwezi Januari. Amewakosoa vikali wale wanaowalaumu Waislamu kuwa wanahusika na hujuma hizo. Aidha amewatuhumu wanasiasa Ufaransa kuwa wanapuuza udhalimu wanaotendewa Waislamu na wala hawachukui hatua zozote za maana kuzuia vitendo hivyo. Kuna takribani Waislamu milioni tano Ufaransa wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za kaskazini mwa Afrika.../mh