IQNA

Binti Mturuki ahifadhi Qur’ani kwa miezi mitatu

14:55 - July 22, 2015
Habari ID: 3332177
Binti Mturuki mwenye umri wa miaka 12 wamefanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu kwa muda wa miezi mitatu tu.

Alif Uzin, anayeishi katika mji wa Karapinar eneo la Konya, Uturuki, ametumia mbinu maalumu ya kuhifadhi, imerioti imesema idara ya masuala ya kidini Uturuki.
Binti huyo amesema walimu wake katika Kituo cha Qur’ani cha Zafari walimsaidia kuhifadhi Qur’ani kwa muda mfupi sana.
Dada yake mkubwa Alif, ambaye pia amehifadhi Qur’ani kikamilifu, anasema binafsi alichukua zaidi ya miezi mitatu kuhifadhi Qur’ani.
Alif anasema sasa baad aya kuhifadhi Qur’ani anataka kutumia wakati wake mwingi akitafakari kuhusu maana na maudhui za kitabu hicho kitakatifu. Binti huyo Mturuki aidha anajitahidi kujifunza kikailifu lugha ya Kiarabu.../mh

3331690

captcha