IQNA

Qur'ani Katika Maisha

Mwanafunzi: Kuhifadhi Qur’ani husaidia mafanikio makubwa shuleni

22:25 - December 23, 2024
Habari ID: 3479941
IQNA – Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 anasema kuhifadhi Quran Tukufu kumemsaidia kupata mafanikio zaidi shuleni.

Katika Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika Tabriz, Iran,  Mohanna Qanbari kutoka Mkoa wa Gilan alipata nafasi ya kwanza katika kitengo cha wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 kwa kuhifadhi Qur'ani nzima.

Akitafakari kuhusu maandalizi yake, Qanbari alisema, "Kwa kawaida mimi hupitia sehemu kadhaa kila siku, na mashindano yanapokaribia, ninafanya mazoezi kupitia vikao vya maswali na majibu na mama yangu."

Safari yake ilianza akiwa na umri wa miaka sita, wakati mama yake alipotambua kipaji chake katika Quran.

Alianza mafunzo maalumu ya kuhifadhi chini ya uongozi wa mwalimu wake, na kufikia umri wa miaka kumi, alikuwa amehifadhi Qur’ani nzima.

Akizungumzia wasiwasi uliopo miongoni mwa baadi kuhusu kuleta mlingano kati y masomo ya Qur'ani na elimu rasmi, Qanbari alisisitiza, "Kwa mipango ifaayo, mtu anaweza kuendeleza masomo ya Qur’ani  na masomo ya shule. Kuhifadhi Qur’ani huongeza kumbukumbu na umakini, hivyo basi kufaulu zaidi katika masomo."

Awali Qanbari aliiwakilisha Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi wa Kiislamu, na kupata nafasi ya kwanza.

Akitazama mbele, analenga kufuata elimu ya juu huku akijiimarisha katika Qur'ani sambamba na kuwafaidisha wengine na ujuzi wake.

Alipoulizwa kuhusu athari za Qur'ani katika maisha yake ikilinganishwa na wenzake, alisema, "Qur'an inafundisha somo la maisha. Kujishughulisha nayo huleta amani ya ndani na kumpa mtu uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha."

Mafanikio yake yamewatia moyo wanafunzi wenzake, ambao wengi wao wamesitawisha shauku ya kujifunza Qur’ani na kuanza safari ya kuihifadhi.

Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yaliyoandaliwa mwezi Disemba na Shirika la Wakfu na Misaada la Iran, ni tukio kubwa zaidi la Qur'ani nchini linalovutia washiriki kote nchini kushindana katika kategoria mbalimbali.

Mashindano hayo yaliyofanyika mapema mwezi huu huko Tabriz, yanalenga kukuza maadili ya Kiislamu, kuimarisha elimu ya Qur'ani, na kusherehekea vipaji vya kipekee. Washindi wakuu wanachaguliwa kuiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani duniani kote.

3491162

Habari zinazohusiana
captcha