IQNA

Vituo 169 vya Qur'ani vyafunguliwa Niger

12:09 - July 27, 2015
Habari ID: 3335751
Shirika moja la kutoa misaada nchini Qatar limeanzisha vituo 169 vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Niger.

Shirika la Misaada la Qatar (QC) limetoa wito kwa wafadhili kuimarisha hali ya Madrassah za Qur'ani (Khalwas) katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika kwa kuwalipa mishahara waalimu na kusambaza nakala zaidi za Qur'ani.
Niger ina madrassaha takribani 50,000 za Qur'ani ambazo ziko katika hali mbaya. Shirika la Misaada la Qatar limeanza kukarabati madrassah hizo kupitia ofisi zake za mji mkuu wa nchi Niger, Niamey.
Idadi kubwa ya madrassah za Qur'ani hazina vyumba vya kusomea na wanafunzi hulazimika kusomea chini ya miti au vibandani jambo ambalo hupelekea wengi kutoenda shuleni au kukabiliwa na matatizo wakati wa kuhifadhi Qur'ani.
Shirika hilo la Qatar  limeazimia kuchukua hatua kadhaa za kuimarisha vituo vya Qur'ani nchini Nigeria ikiwa ni pamoja na kusambaza nakala 10,000 za Qur'ani Tukufu.../mh

3335568

captcha