Waathiriwa walipoteza maisha katika shambulio la kikatili la silaha katika mtaa wa Fambita wa mji wa mpakani wa vijijini wa Kokorou, wizara ya mambo ya ndani ilisema katika taarifa iliyotangazwa kwenye televisheni ya serikali Ijumaa.
Wizara ilisema watu wengine 13 walijeruhiwa.
Ukanda wa Sahel wa Afrika Magharibi umeshuhudia ongezeko la vurugu katika miaka ya hivi karibuni kufuatia kuibuka magaidi wanaokufurisha Waislamu wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya al-Qaeda na Daesh (ISIL au ISIS) ambayo yalianza kuene maeneo kaskazini mwa Mali baada ya uasi wa kabila la Tuareg wa mwaka 2012.
Tangu wakati huo, vurugu zimeenea nchini jirani Niger na Burkina Faso, na karibuni zaidi kuelekea kaskazini mwa nchi za pwani za Afrika Magharibi kama Togo na Ghana.
Wizara ya mambo ya ndani ya Niger ilisema shambulio hilo la karibuni lilitokea mapema alasiri huku watu wakiwa wanahudhuria sala msikitini wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
"Majambazi waliokuwa na silaha nzito walizingira msikiti ili kutekeleza mauaji yao kwa ukatili wa ajabu," wizara ilisema, ikiongeza kuwa washambuliaji hao pia waliteketeza soko la ndani na nyumba.
Wizara ya ulinzi ililaumu shambulio hilo kwa Daesh katika Jangwa Kubwa, au EIGS, mshirika wa Daesh, katika taarifa iliyotolewa Ijumaa usiku.
EIGS haikutoa majibu yoyote ya haraka kuhusu madai hayo. Mashambulio ya awali nchini Niger yalidaiwa kufanywa na makundi washirika wa al-Qaeda.
Serikali imeahidi kuwafuatilia wahalifu na kuwafikisha mahakamani.
Serikali inayoendeshwa kijeshi ya Niger mara kwa mara inapambana na makundi yenye silaha katika eneo hilo, huku raia mara nyingi wakiwa waathiriwa wa vurugu hizo.
Tangu Julai 2023, takriban watu 2,400 wameuawa nchini Niger, kulingana na hifadhidata ya ACLED, shirika lisilo la kiserikali linalotoa data za matukio ya mizozo yenye silaha.
Katika eneo kubwa la Sahel linalojumuisha nchi kadhaa, mamia ya maelfu zaidi wameuawa na mamilioni wamefurushwa makwao huku makundi yenye silaha yakishambulia miji na vijiji pamoja na vituo vya usalama vya serikali.
Kushindwa kwa serikali kurejesha usalama kumechangia mapinduzi mawili nchini Mali, mawili Burkina Faso na moja Niger kati ya 2020 na 2023. Nchi zote tatu bado ziko chini ya utawala wa kijeshi licha ya shinikizo la kikanda na kimataifa la kufanyika kwa uchaguzi.
3492471