IQNA

Njama za Wamagharibi

Sheikh Zakzaky aonya kuhusu njama za Marekani, Ufaransa kuibua mifarakano baina ya Niger, Nigeria

12:49 - August 20, 2023
Habari ID: 3477465
ABUJA (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) ametahadharisha juu ya njama na majungu yanayopikwa na Marekani na Ufaransa ya kupanda mbegu za chuki, uhasama na mifarakano baina ya Nigeria na jirani yake Niger.

Sheikh Ibrahim Zakzaky ametoa indhari hiyo Jumamosi akihutubia wanafunzi wa Hauza ya Kiislamu mjini Abuja na kueleza kuwa, Washington na Paris zinafanya juu chini kuibua uhasama baina ya nchi mbili hizo jirani za Afrika Magharibi.

Sheikh Zakzaky ameeleza bayana kuwa, "Licha ya Niger kufunga anga yake, lakini ndege za Ufaransa zinaruka (katika anga hiyo). Ufaransa imeendelea kusimamia kambi za magaidi nchini Niger, na hilo ndilo chimbuko la mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram wenye mfungamano na Daesh."

Mwanachuoni huyo wa Kiislamu nchini Nigeria amebainisha kuwa, magaidi hao wanafanya mashambulizi sambamba na kuiba rasimimali za madini kama dhahabu na kisha kugawana na mabwana zao.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa, huenda magaidi hao wakatumiwa pia kufanya mashambulizi dhidi ya Abuja, ili Niamey ilaumiwa na kinyume chake.

"Kwa msingi huo, hatua yoyote ya kijeshi katika mipaka ya nchi mbili (Nigeria na Niger) itatokana na uhandisi wa Marekani na Ufaransa, na wala si Nigeria na Niger, " amesema Sheikh Zakzaky.

Kiongozi huyo mashuhuri wa kidini nchini Nigeria amesema huenda madola hayo ya kikoloni yakaibua vita na mizozo ya kikabila nchini Niger, kama walivyofanya Sudan. 

Onyo la Zakzaky limekuja baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kusema nchi wanachama zimeafikiana juu ya kuiingilia kijeshi Niger, ili kumrejesha Rais Mohammed Bazoum aliyepindukiwa Julai 26.

3484840

Kishikizo: niger nigeria
captcha