IQNA

Adebayor afafanua sababu za kuukubali Uislamu

20:05 - August 04, 2015
Habari ID: 3338997
TEHRAN (IQNA)- Mwezi moja baada ya kutangaza kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu, Emmanuel Adebayor, mchezaji soka mashuhuri Mwafrika nchini Uingereza ambaye sasa ni mshambuliaji wa Tottenham, amefafanua sababu zilizompelekea kusilimu.

Adebayor amenukuliwa  na tovuti ya On Islam akisema: “Nabii Issa AS (Yesu) alifundisha kuwa Mungu ni Mmoja na anapaswa kuabudiwa kama ilivyo katika Bibilia, Kumbukumbu la Torati 6:4 na Marko 12:29. Waislamu pia wanaitikadi hivyo kama ilivyo katika Qur’ani Tukufu Sura ya 4:171” Adebayo ametoa sababu 13 zilizompelekea kuukumbatua Uislamu; hii ni baada ya kuonekana katika tovuti ya You Tube akitamka Shahada. Akiwa amevalia kanzu nyeupe, Adebayo anasikika akisilimu kwa kutamka shahada  ya ‘Hakuna Apasaye Kuabudiwa ila Allah na Mohammad Ni Mtume Wake ’. Amesema moja ya sababu ya kusilimu kwake ni kuwa Nabii Issa AS hakuwahi kula nyama ya nguruwe kama ambavyo leo Waislamu hawali nyama  hiyo. Adebayor ambaye ni raia wa Togo anasema maneno kama vile As Salaamu Alaikum na Inshallah ambayo yametajwa katika Qur’ani Tukufu yalikuwa pia yakitumiwa na Nabii Issa AS.
Adebayor anaongeza kuwa,“Nabii Issa AS alikuwa akiosha uso, mikono na miguu yake kabla ya kusali. Waislamu wanafanya hivyo pia. Nabii Issa AS na Mitume wengine walisujudu ardhini (Mathayo 26:39). Waislamu nao pia wamefundishwa kufanya hivyo katika Qur’ani Tukufu Sura za 3:84 na 2:285.”
Adebayo aliwahi kuchezea timu kadhaa za soka ikiwani ni pamoja na Metz na Monaco nchini Ufaransa, Arsenal na Manchester City nchini Uingereza na Real Madrid huko Uhispania. Aidha aliwahi kutangazwa mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika mwaka 2008. Nukta nyingine ilivyomvutia Adebayor katika Uislamu ni kujistiri Bibi Maryam, Mama wa Nabii Issa Masih AS ambaye alikuwa na mavazi yaliyomfunika mwili wote na pia mtandio kichwani, mavazi ambayo wanawake Waislamu wanayavaa hadi leo. Sababu nyingine ilivyomvutia Adebayor katika Uislamu ni namna Waislamu wanavyofungamana kikamilifu na funga au saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyoamurishwa katika Bibilia na Qur’ani Tukufu.Halikadhalika mchezaji huyo mashuhuri wa soka anagusia adabu za Kiislamu kama vile kusema ‘Bismillah’ au Kwa Jina la Allah kuwa nukta nyingine iliyompelekea aukumbatie Uislamu maishani. Adebayo pia anasema mila na desturi ya Waislamu kusisitiza ulazima wa kuwatahiri watoto wa kiume kuwa ni nukta inayoashiria kufungamana na mafundisho ya Nabii Issa AS.
“Nabii Issa AS alizungumza lugha ya Aramaic na alimuita Mwenyezi Mungu “Elah” ambayo tamko lake ni sawa na Allah Kwa Kiarabu. Aramaic ni lugha ya kale ya Bibilia,” amenukuliwa akisema Adebayor. Mchezaji huyo wa soka mwenye umri wa miaka 31 na ambaye ametajwa kuwa  kuwa mwenye kufungamana na mafundisho ya dini amnukuliwa akisema, “Sasa nifahamishe ni nani mfuasi halisi wa Nabii Issa AS? Bila shaka ni Waislamu. Kwa hivyo naamini kuwa mimi ni mfuasi halisi wa Nabii Issa AS.../mh

3338700

captcha