IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yafanyika Afrika Kusini

16:04 - September 02, 2015
Habari ID: 3357512
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamefanyika Afrika Kusini kwa usimamizi wa Idara ya Masuala ya Qur'ani nchini humo.

Kwa mujibu wa hqmi.org mashindano hayo yamefanyika kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Qur'ani.

Imearifiwa kuwa wanaharakati 43 wa Qur'ani walishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani nzima na kuhifadhi Juzuu 15 na 5.
Washindi walitunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika katika Msikiti wa Al Fath  mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Sheikh Riyadh Fatar, Naibu Mkuu wa  Baraza la Sheria za Kiislamu mjini Cape Town pamoja na wawakilishi wa taasisi kadhaa za Kiislamu, waalimu wa Qur'ani na wanafunzi.
Wazunggumzaji katika kikao hicho wamesisitiza umuhimu wa fadhila za kuhifadhi Qur'ani na athari zake nzuri kwa wanaohifadhi miongoni mwa Waislamu Afrika Kusini.../mh

3354490

captcha