IQNA

Qarii wa kimataifa wa Iran ni miongoni mwa walipoteza maisha Mina

13:45 - September 26, 2015
Habari ID: 3370739
Qarii mashuhuri wa Iran aliokuwa katika msafara wa Qur'ani wa mahujaji amethibitishwa kuaga dunia kufuatia msongamano mkubwa wa mahujaji katika eneo la Mina karibu na mji mtakatifu wa Makka.

Mohsen Hajihassani Kargar ambaye alichukua nafasi ya kwanza katika Mashindano ya 57 ya Kimatiafa ya Qur’ani Malaysia mwezi Juni mwaka huu alikuwa kati ya mahujaji Wairani waliotangazwa kutoweka kufuatia maafa ya Mina siku ya Alkhamisi. Ndugu yake, Mostafa Hajihassani Kargar amethibitisha kupokea habari ya kusikitisha ya kifo cha ndugu yake.
Zaidi ya mahujaji 1,300 wakiwemo Wairani 131 wamethibitishwa kupoteza maisha hadi sasa katika maafa ya Mina ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni katika Hija.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei siku ya Alkhamisi alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa ya Mina.../mh

3369395

captcha