IQNA

UN yataka Waislamu Myanmar waruhusiwe kupiga kura

13:15 - October 31, 2015
Habari ID: 3421779
Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa Myanmar itakumbwa na mgogoro mkubwa iwapo uchaguzi wa wiki ijayo hautazingatia vigezo muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapa Waislamu haki ya kupiga kura.

Yanghee Lee mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar amesema mamia ya wagombea wamenyimwa haki ya kigombea huku mamili ya maelfu wakinymwa haki ya kupiga kura hasa Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine na vile vile Wamyanmar wenye asili ya China na India.
Ikiwa imebakia wiki moja kabla ya uchaguzi nchini Myanmar, viongozi mabudha wa nchi hiyo wamesema kuwa, Waislamu wa kabila la Rohingya hawana haki ya kupiga kura.
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa vyombo vya habari hususan vya Magharibi vimekuwa vikieneza propaganda kuwa uchaguzi wa Bunge nchini Miyanmar utafanyika katika anga huru na kushirikisha vyama vyote, makundi yote ya kikabila, mbari na watu wa dini zote. Juhudi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) zilizaa matunda kiasi kwamba ilikuwa imekubaliwa kuwa, Waislamu wenye kadi za kupigia kura wangeliruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo. Hata hivyo kiongozi mmoja mwandamizi wa Chama cha Taifa kwa ajili ya Demokrasia cha Bi Aung San Suu Kyi ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Myanmar amefichua kuwa, mamia ya maelfu ya Waislamu wa Rohingya wamepigwa marufuku kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa sababu za kidini na kikabila. Hata Waislamu ambao wamepewa kadi za kupigia kura hawathaminiwi na chama chochote kinachoshiriki kwenye uchaguzi huo. Jambo la kustaajabisha zaidi ni kuwa, chama kikuu cha upinzani na vyama vingine vya Myanmar vimeundwa kwa misingi ya kikabila. Chama hicho cha Harakati ya Taifa kwa ajili ya Demokrasia kinaundwa na makundi ya mabudha yenye misimamo mikali mno ambayo yanaendesha kampeni za kuwaangamiza Waislamu wote nchini humo. Chama hicho kina wagombea 151 kutoka maeneo yote ya Myanmar, lakini hakuna hata Muislamu mmoja kwenye orodha ya wagombea hao. Chama hicho kiko tayari kufanya jambo lolote lile lenye madhara kwa Waislamu alimradi tu kilinde uluwa wake katika medani ya kisiasa nchini Myanmar. Katika miezi ya hivi karibuni pia, mkuu wa chama hicho Bi Aung San Suu Kyi alichukua hatua kadhaa za kuwakandamiza Waislamu na kuwafanya wahanga wa malengo yake ya kisiasa.
Ni jambo linalofaa kusisitiziwa hapa kwamba, Myanmar ina historia ya kutawaliwa na majenerali madikteta wa kijeshi. Hata Rais Thein Sein wa Myanmar alikuwa kamanda wa jeshi kabla ya kuvua magwanda na kujivika joho la siasa. Hivyo hata chama tawala cha Mshikamano ambacho kinajionesha kuwa si cha kijeshi, kimeandaa mazingira mazuri ya kukandamizwa Waislamu.
Amma cha kusikitisha zaidi ni kuona kuwa madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yanaiona Myanmar ni kama nembo ya uhuru na ukombozi. Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana madola hayo ya Magharibi yako tayari kukabiliana na hatua zozote za kuwashinikiza watawala wa Myanmar licha ya ukandamizaji mkubwa wanaowafanyia Waislamu. Ni kwa sababu hiyo pia ndio maana tunaweza kusema kwa kifua kipana kwamba, nchi za Magharibi ndiyo sababu kuu ya kuendelea unyanyasaji nchini Myanmar. Kama ambavyo pia; mamia ya maelfu ya Waislamu wa Myanmar wamekuwa wakifanyiwa ukatili mkubwa kwa sababu tu ya kupigania haki zao za kimsingi, lakini si Magharibi tu, bali mashirika yao ya haki za binadamu nayo yameshindwa kuchukua hatua zozote za maana za kuwalinda na kuwatetea Waislamu hao, na hilo linazidi kudhihirisha sura halisi ya kindumilakuwili ya madola Magharibi na mashirika yao ya kutetea haki za binadamu.

3421606

captcha