IQNA

Iran yawasilisha azimio UN kupinga misimamo mikali duniani

22:47 - December 12, 2015
Habari ID: 3462298
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha kwenye Baraza Kuu la umoja huo rasimu ya azimio lililopendekezwa na Jamhuri ya Kiislamu la 'dunia isiyo na ukatili na vitendo vya kufurutu mpaka'.

Akizungumza Alhamisi katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) Gholamali Khoshroo, amesema kuwa na kauli moja na kuunga mkono nchi wanachama azmio hilo lililopendekezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ushahidi na ithbati juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua na Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na changamoto ya 'vitendo vya ukatili na msimamo ya kufurutu ada ya utumiaji mabavu' duniani.

Huku akisisitiza kuwa misimamo ya kufurutu mpaka ya ukatili na utumiaji mabavu haina nafasi katika dini za tauhidi, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa kukoleza moto wa ubaguzi, uenezaji chuki na kuzusha tuhuma dhidi ya wafuasi wa dini nynginezo hakutokuwa na matunda mengine zaidi kuzipa nguvu fikra pofu na za ukatili na utumiaji mabavu za magaidi.

Amesisitiza pia juu ya nukta kwamba katika dunia ya leo vitisho vya kigaidi havina mpaka wowote wa kijiografia na kuongeza kuwa njia pekee ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kuwepo jitihada za pamoja za Jamii ya Kimataifa.

3462141

captcha