Mashindano hayo yameanza kwa qiraa ya Qur’ani Tukufu ya qarii mashuhuhuri Muirani Sayyed Jawad Husseini.
Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa kisiasa, kiutamaduni pamoja na wataalamu bingwa wa Qur’ani Tukufu.
Kuna washiriki zaidi ya 630 wakiwemo maqarii na waliohifadhi Qur’ani kutoka maeneo yote ya Iran watakaoshiriki katika mashindano hayo ya wiki moja.
Kwa mujibu wa mkuu wa Kitengo cha Qur’ani katika Shirika la Awqaf la Iran Hujjatul Islam Seyed Mustafa Husseini, mbali na mashindano hayo kutakuwa pia na warsha 40 za Qur’ani na vikao 86 vya qiraa ya Qur’ani pembizoni mwa mashindano hayo.
Mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Iran kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuvumbua vipaji vya Qur’ani miongoni mwa washiriki na vilevile kuimarisha na kustawisha utamaduni na harakati za Qur’ani nchini.