Fatima Dehqan, 16, anashindana katika kategoria ya qiraa katika sehemu ya wanawake ya mashindano ya mwaka huu.
Alianza kujifunza usomaji wa Qur'ani na Tajweed akiwa na umri wa miaka kumi.
Mbali na qiraa, anajifunza kuhifadhi Qur'ani na a hadi sasa amehifadhi Juzuu 10.
Akizungumza Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), baada ya kupanda jukwaani katika mashindano hayo, Fatima alisema hutumia saa nne hadi tano kwa siku kuhifadhi Qur'ani na kuimarisha ujuzi wake wa kusoma.
Alipoulizwa iwapo qari pia anafaa kuwa mhifadhi wa Quran, alisema haikuwa lazima, lakini baada ya kugundua kuwa ana nia ya kuhifadhi Quran na ana uwezo huo, aliamua kufanya hivyo.
Pia alisema kwamba muda unaotumika katika kujifunza Qur'ani haumzuii kusoma masomo yake ya shule.
“Marafiki zangu huniuliza ninawezaje kufanya shughuli zote hizi na ninawaambia ni baraka za Kimungu.”
Kwingineko katika maelezo yake, Fatima aligusia nafasi ya wazazi wake katika kumsaidia kuvumbua vipaji vyake vya Qur'ani na akasema walifanya juhudi nyingi kumsaidia kufaulu katika nyanja za Qur'ani.
Fatima pia alisema anapenda kuhudumu kama mjumbe wa jopo la majaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani atakapokuwa mkubwa.
Kuhusu kazi ya ndoto yake, alisema angependa kuwa mwalimu wa lugha ya Kiarabu.
Duru ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran inaendelea katika mji wa kaskazini-magharibi wa Tabriz.
Jumla ya washiriki 225 wamefuzu kwa hatua ya fainali itakayoendelea hadi Desemba 19 huko Tabriz.
Tukio la mwaka huu linafanyika kwa kauli mbiu ya "Mashahidi wa Huduma," ikiwa ni pamoja na Rais wa zamani Ebrahim Raisi na wenzake, ambao walipoteza maisha yao katika ajali ya helikopta mwezi Mei.
Washindi wa mashindano hayo wataiwakilisha Iran katika matukio ya kimataifa ya Qur'ani kote duniani.
3490974