IQNA

9:00 - January 06, 2016
Habari ID: 3470018

Jumuiya 55 za Mauritania zataka taasisi za Qur’ani zifunguliwe

Jumuiya 55 nchini Marutania zimetoa taarifa na kuwataka wakuu wa nchi hiyo kufungua tena taasisi na shule za Qur’ani nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti la al Akhbar, jumuiya hizo zimeitaka serikali kuondoa masharti makali ya kufungua taasisi za Qur’ani ambazo zilifungwa hivi karibuni kwa kisingizio cha kueneza misimamo mikali na kufanya kazi bila vibali.

Ikumbukwe kuwa Desemba mwaka jana, kulifanyika maandamano maeneo kadhaa ya Mauritania kulaani hatua ya serikali kufunga vituo kadhaa vya Qur’ani na chekechea.

Viongozi wa kidini na wahubiri nchini humo nao pia wameonya kuhusu kuvurugwa masomo ya kidini na Qur’ani nchini humo.

Mauritania ni nchi ya eneo la Maghreb huko magharibi mwa Afrika Kaskazini na inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4 ambao karibu wote ni Waislamu.

3464407

captcha